Tuesday, August 13, 2013

WILAYA YA CHUNYA - MAUAJI.



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 13. 06. 2013.


WILAYA YA  CHUNYA  - MAUAJI.

MNAMO TAREHE 12.08.2013 MAJIRA YA  SAA 16:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITINDI WILAYA YA  CHUNYA MKOA WA MBEYA. HATIBU S/O MWAKALINGA, MIAKA 36, KYUSA, MVUVI, MKAZI WA KIJIJI CHA ITINDI ALIUAWA KWA KUPIGWA FIMBO MBAVUNI NA WACHUNGAJI NG’OMBE WAFUGAJI WA KISUKUMA. MAREHEMU ALIKUWA NA KUNDI LA SUNGUSUNGU WAKIKAMATA MIFUGO MALI YA WAFUGAJI WALIOFAHAMIKA KWA JINA MOJA MOJA 1. MWANAHELA S/O ? 2.  KABAHUNGU S/O ? NA 3. LUKANGILA  S/O ?.  MIFUGO HIYO ILIKUWA INAKULA MAZAO KATIKA SHAMBA LA MKULIMA AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA. MIFUGO ILITOROSHWA MARA BAADA YA  TUKIO HILO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI  YA  MWAMBANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.

WILAYA YA  MBEYA VIJIJINI – AJALI YA  MOTO NA KUSABABISHA VIFO.


MNAMO TAREHE 12.08.2013 MAJIRA YA  SAA 07:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MSHEWE KATA YA  UTENGULE USONGWE WILAYA YA  MBEYA VIJIJINI  MKOA WA MBEYA. RAPHAEL S/O MBWIGA,MIAKA 22, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA MSHEWE, AKIWA MNADANI KATIKA SHUGHULI ZAKE ZA KIBIASHARA  ALIPATA TAARIFA ZA KUUNGUA KWA NYUMBA YAKE NA KUSABABISHA VIFO VYA WATOTO WAKE WAWILI 1.DESMOS S/O RAPHAEL,MIAKA 2 NA MIEZI 7,MSAFWA NA 2. DORCAS D/O RAPHAEL, MIEZI 4, MSAFWA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA MSHEWE. CHANZO NI BAADA YA  MAMA MZAZI WA MAREHEMU HAO FLOIZA D/O EMANUEL, MIAKA 20, MSAFWA, MKULIMA,  MKAZI WA KIJIJI CHA MSHEWE AMBAYE ALIKUWA AMELALA NA WATOTO WAKE ALITOKA  NJE MAJIRA YA  SAA 06:00HRS KUJISAIDIA NA KUACHA AMEWASHA KIBATARI NA ALIPORUDI ALIKUTA MOTO UNAWAKA NA KUTEKETEZA VYUMBA VIWILI KIKIWEMO WALICHOKUWA WAMELALA WATOTO WAKE. MOTO HUO ULIZIMWA NA MAJIRANI. NYUMBA HIYO ILIKUWA NA VYUMBA VIWILI IMEJENGWA KWA MATOFALI MABICHI NA KUEZEKWA NYASI. THAMANI HALISI YA  MALI ILIYOTEKETEA BADO KUJULIKANA. MIILI YA  MAREHEMU IMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUZIKWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI KATIKA MAJANGA YA  MOTO ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.

WILAYA YA  RUNGWE – KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 12.08.2013 MAJIRA YA  SAA 09:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISANGE KATA YA  ISANGE WILAYA YA  RUNGWE MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA EMANUEL S/O MWAISOBWA,MIAKA 35,KYUSA,MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ISANGE AKIWA NA BHANGI KILO MOJA. MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI.TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.



WILAYA YA  CHUNYA – KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 12.08.2013 MAJIRA YA  SAA 17:00HRS HUKO KATIKA  MTO LILONGO- MKWAJUNI WILAYA YA  CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA SONAMA S/O HAJI, MIAKA 34,MNGONI,MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA MKWAJUNI  AKIWA NA BHANGI GRAMU 500. MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI.TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.


WILAYA YA  CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO]

MNAMO TAREHE 12.08.2013 MAJIRA YA  SAA 14:30HRS HUKO KATIKA  KIJIJI CHA KAMBI KATOTO WILAYA YA  CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA CHIKU D/O ABDULA, MIAKA 26,MSANGU,MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KAMBI KATOTO  AKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 20. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI

WILAYA YA  CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO]

MNAMO TAREHE 12.08.2013 MAJIRA YA  SAA 12:30HRS HUKO KATIKA  KIJIJI CHA KAMBI KATOTO WILAYA YA  CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JILATU S/O NKIBU, MIAKA 52,MSUKUMA,MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KAMBI KATOTO  AKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 20. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.





 [ DIWANI ATHUMANI   - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


No comments: