Saturday, August 17, 2013

WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 17. 08. 2013.



WILAYA YA  MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO]

MNAMO TAREHE  16.08.2013 MAJIRA YA  SAA 16:15HRS HUKO ENEO LA MAKUNGURU JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1. ANATARIA D/O MATUMA, MIAKA 24,KYUSA,MKULIMA  2. NOAH S/O MWANGOKA, MIAKA 31,KYUSA,MKULIMA NA 3. MASUMBUKO S/O JAILOS, MIAKA 28,MSAFWA,MKULIMA WOTE WAKAZI WA MAFIATI WAKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 3,  WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII  KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.



                                                               
 [DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

‘POLISI JAMII CUP’

 TANGAZO                TANGAZO                       TANGAZO

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI ATHUMANI – ACP KWA KUPITIA KITENGO CHA POLISI JAMII KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALIMBALI. ANAYO FURAHA KUBWA KUWAALIKA WAKAZI WOTE WA JIJI LA MBEYA KUSHUHUDIA FAINALI YA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU ‘POLISI JAMII CUP’ AMBAYO YALIANZA TAREHE 10/08/2013 NA KILELE CHAKE NI KESHO SIKU YA TAREHE 18/08/2013 MAJIRA YA SAA 10:00 JIONI KATIKA VIWANJA VYA SHULE YA MSINGI RWANDA – NZOVWE. MGENI RASMI ATAKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

WOTE MNAKARIBISHWA.

WILAYA YA MBARALI – MAUAJI.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 16. 08. 2013.


WILAYA YA  MBARALI – MAUAJI.


MNAMO TAREHE  14.08.2013  MAJIRA YA  SAA 03:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MADABAGA WILAYA YA  MBARALI MKOA WA MBEYA. DOTO S/O SODELA, MIAKA 26, MKULIMA, MSUKUMA,MKAZI WA KIJIJI CHA MADABAGA ALIUAWA KWA KUPIGWA FIMBO KICHWANI NA NDUGU ZAKE. CHANZO NI BAADA YA  MAREHEMU KUKATAA KUKAMATWA MAJIRA YA  SAA 23:00HRS KWA TUHUMA ZA KUTAKA KUMBAKA WAYAGA D/O MWINANIRA, MIAKA 14, MKULIMA/MFUGAJI, MSUKUMA MKAZI WA KIJIJI CHA MADABAGA WAKATI AKIWA MACHUNGANI MAJIRA YA  SAA 16:30HRS . WATUHUMIWA WATANO WAMEKAMATWA AMBAO NI 1.MUONDELA S/O JINAI,MIAKA 30, MSUKUMA, MKULIMA  2.SHIGELA S/O SODELA, MIAKA 33, MSUKUMA, MKULIMA 3.GERE S/O MWINANIRA, MIAKA 39, MSUKUMA, MKULIMA 4.MOSHILO S/O MWINANIRA, MIAKA 22, MSUKUMA, MKULIMA NA 5.VENGO S/O SODELA, MIAKA 29, MSUKUMA, MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA MADABAGA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI.TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI .KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII  KUTOJICHULIA SHERIA MKONONI BADALA YAKE WAWAFIKISHE KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

WILAYA YA  MBOZI – AJALI YA  MAGARI MAWILI KUGONGANA NA TREKTA NA
                                           KUSABABISHA VIFO
NA MAJERUHI.

MNAMO TAREHE 15.08.2013 MAJIRA YA  SAA 20:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHIMBUYA BARABARA YA  MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA  MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI T.765 BBA AINA YA  SCANIA LILILOKUWA LIKITOKEA MBEYA MJINI KUELEKEA TUNDUMA LILIENDESHWA NA DEREVA AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE LILIGONGA  TREKTA AMBALO HALIJAFAHAMIKA NAMBA ZA USAJILI KISHA KULIGONGA GARI ACP 8839 AINA YA  SCANIA  MALI YA  KAMPUNI YA  USAFIRISHAJI YA  DHANDHO LILILOKUWA LIKITOKEA TUNDUMA KUELEKEA MBEYA MJINI DEREVA WA GARI HILO BADO KUFAHAMIKA. KATIKA AJALI HIYO WATU WATATU  WAWILI KATI YAO WALIKUWA KATIKA GARI T.765 BBA NA MMOJA NI DEREVA WA TREKTA  AMBAO HAWAJATAMBULIKA MAJINA WALA MAKAZI YAO,  WOTE WANAUME WALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO.  AIDHA WATU WAWILI  WALIOKUWA KATIKA GARI ACP 8839 AMBAO PIA HAWAJATAMBULIKA WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA  KATIKA HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA.  MIILI YA  MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA  SERIKALI VWAWA WILAYA YA  MBOZI. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.




                                                                Signed by:
 [DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

WILAYA YA MBEYA MJINI – UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA [PANGA].

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 15. 08. 2013.


WILAYA YA  MBEYA MJINI – UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA [PANGA].



MNAMO TAREHE 14.08.2013 MAJIRA YA SAA 16:50HRS HUKO AIRPORT - TANKINI JIJI NA MKOA WA MBEYA.  DANIEL S/O SONGELA, MIAKA 24, KYUSA, DEREVA WA PIKIPIKI @ BODABODA, MKAZI WA ZZK-MBALIZI,  ALINYANG’ANYWA PIKIPIKI YAKE T.691 CJF AINA YA  KINGLION  NA WATU WAWILI. MBINU NI KUKODIWA NA MTEJA  MMOJA KWA UJIRA WA TSHS 5,000/= KUTOKA MBALIZI HADI ENEO LA ESSO NA NJIANI WALIKUTANA NA MTU MWINGINE ALIYEVAA SARE ZA JWTZ AKIWA AMESHIKA PANGA HIVYO WALIFANIKIWA KUMPORA MHANGA PIKIPIKI HIYO. KUFUATIA TUKIO HILO JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WAENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA LILIFANYA MSAKO NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WAWILI 1. BARAKA S/O DAUDI, MIAKA 20, KYUSA, BIASHARA MKAZI WA MAMA JOHN NA 2.SHADRACK S/O ESSAU, MIAKA 21, BIASHARA , MKAZI WA MWAMBENE WAMEKAMATWA NA KUKIRI KUHUSIKA KATIKA MATUKIO YA  UPORAJI WA PIKIPIKI MAENEO MBALIMBALI. JUMLA YA PIKIPIKI NANE ZINAZODHANIWA KUWA MALI YA WIZI ZIMEKAMATWA KATIKA MSAKO HUKO TUKUYU WILAYA YA RUNGWE NA WATUHUMIWA SITA WAMEKAMATWA 1.SIMON S/O MWANYASI, MIAKA 35, KYUSA, MKULIMA 2.LWITIKO S/O HADSON, MIAKA 22, KYUSA, MKULIMA 3. OSFA S/O MWAMAKULA, MIAKA 38, KYUSA, MKULIMA 4.FESTO S/O GIDEON, MIAKA 35, KYUSA, MKULIMA 5.SOFIA D/O GIDEON, MIAKA 35, KYUSA, MKULIMA NA 6.NOEL S/O YESAYA, MIAKA 34, KYUSA, MKULIMA WOTE WAKAZI WA TUKUYU. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII  KUACHA TABIA YA  KUJIPATIA KIPATO / MALI KWA NJIA YA  MKATO KWA TAMAA YA  UTAJIRI WA HARAKA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA  BADALA YAKE WAJISHUGHULISHE NA SHUGHULI HALALI ZA KUJIPATIA KIPATO. AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WALIOWAHI KUIBIWA AU KUPOTELEWA PIKIPIKI ZAO KUFIKA KITUO CHA POLISI KATI MBEYA KWA AJILI YA  UTAMBUZI WA MALI ZAO.



Imesainiwa na,
 [DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Tuesday, August 13, 2013

WILAYA YA CHUNYA - MAUAJI.



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 13. 06. 2013.


WILAYA YA  CHUNYA  - MAUAJI.

MNAMO TAREHE 12.08.2013 MAJIRA YA  SAA 16:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITINDI WILAYA YA  CHUNYA MKOA WA MBEYA. HATIBU S/O MWAKALINGA, MIAKA 36, KYUSA, MVUVI, MKAZI WA KIJIJI CHA ITINDI ALIUAWA KWA KUPIGWA FIMBO MBAVUNI NA WACHUNGAJI NG’OMBE WAFUGAJI WA KISUKUMA. MAREHEMU ALIKUWA NA KUNDI LA SUNGUSUNGU WAKIKAMATA MIFUGO MALI YA WAFUGAJI WALIOFAHAMIKA KWA JINA MOJA MOJA 1. MWANAHELA S/O ? 2.  KABAHUNGU S/O ? NA 3. LUKANGILA  S/O ?.  MIFUGO HIYO ILIKUWA INAKULA MAZAO KATIKA SHAMBA LA MKULIMA AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA. MIFUGO ILITOROSHWA MARA BAADA YA  TUKIO HILO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI  YA  MWAMBANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.

WILAYA YA  MBEYA VIJIJINI – AJALI YA  MOTO NA KUSABABISHA VIFO.


MNAMO TAREHE 12.08.2013 MAJIRA YA  SAA 07:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MSHEWE KATA YA  UTENGULE USONGWE WILAYA YA  MBEYA VIJIJINI  MKOA WA MBEYA. RAPHAEL S/O MBWIGA,MIAKA 22, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA MSHEWE, AKIWA MNADANI KATIKA SHUGHULI ZAKE ZA KIBIASHARA  ALIPATA TAARIFA ZA KUUNGUA KWA NYUMBA YAKE NA KUSABABISHA VIFO VYA WATOTO WAKE WAWILI 1.DESMOS S/O RAPHAEL,MIAKA 2 NA MIEZI 7,MSAFWA NA 2. DORCAS D/O RAPHAEL, MIEZI 4, MSAFWA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA MSHEWE. CHANZO NI BAADA YA  MAMA MZAZI WA MAREHEMU HAO FLOIZA D/O EMANUEL, MIAKA 20, MSAFWA, MKULIMA,  MKAZI WA KIJIJI CHA MSHEWE AMBAYE ALIKUWA AMELALA NA WATOTO WAKE ALITOKA  NJE MAJIRA YA  SAA 06:00HRS KUJISAIDIA NA KUACHA AMEWASHA KIBATARI NA ALIPORUDI ALIKUTA MOTO UNAWAKA NA KUTEKETEZA VYUMBA VIWILI KIKIWEMO WALICHOKUWA WAMELALA WATOTO WAKE. MOTO HUO ULIZIMWA NA MAJIRANI. NYUMBA HIYO ILIKUWA NA VYUMBA VIWILI IMEJENGWA KWA MATOFALI MABICHI NA KUEZEKWA NYASI. THAMANI HALISI YA  MALI ILIYOTEKETEA BADO KUJULIKANA. MIILI YA  MAREHEMU IMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUZIKWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI KATIKA MAJANGA YA  MOTO ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.

WILAYA YA  RUNGWE – KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 12.08.2013 MAJIRA YA  SAA 09:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISANGE KATA YA  ISANGE WILAYA YA  RUNGWE MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA EMANUEL S/O MWAISOBWA,MIAKA 35,KYUSA,MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ISANGE AKIWA NA BHANGI KILO MOJA. MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI.TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.



WILAYA YA  CHUNYA – KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 12.08.2013 MAJIRA YA  SAA 17:00HRS HUKO KATIKA  MTO LILONGO- MKWAJUNI WILAYA YA  CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA SONAMA S/O HAJI, MIAKA 34,MNGONI,MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA MKWAJUNI  AKIWA NA BHANGI GRAMU 500. MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI.TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.


WILAYA YA  CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO]

MNAMO TAREHE 12.08.2013 MAJIRA YA  SAA 14:30HRS HUKO KATIKA  KIJIJI CHA KAMBI KATOTO WILAYA YA  CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA CHIKU D/O ABDULA, MIAKA 26,MSANGU,MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KAMBI KATOTO  AKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 20. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI

WILAYA YA  CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO]

MNAMO TAREHE 12.08.2013 MAJIRA YA  SAA 12:30HRS HUKO KATIKA  KIJIJI CHA KAMBI KATOTO WILAYA YA  CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JILATU S/O NKIBU, MIAKA 52,MSUKUMA,MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KAMBI KATOTO  AKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 20. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.





 [ DIWANI ATHUMANI   - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 12. 08. 2013. WILAYA YA MBOZI – AJALI YA PIKIPIKI KUGONGANA NA KUSABABISHA KIFO. MNAMO TAREHE 11.08.2012 MAJIRA YA SAA 17:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA WASA KATA YA MSIA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. PIKIPIKI T.225 BNY NA T.758 CCC ZOTE AINA YA T-BETTER ZILIGONGANA NA KUSABABISHA MWENDESHA PIKIPIKI MMOJAWAPO AITWAE ADAM S/O SIMKOKO, MIAKA 27, MNYIHA, MKAZI WA KIJIJI CHA WASA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. CHANZO NI MWENDO KASI KWA WAENDESHA PIKIPIKI WOTE WAWILI. MWENDESHA PIKIPIKI WA PILI HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE BAADA YA KUKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA KUITELEKEZA PIKIPIKI YAKE ENEO LA TUKIO. PIKIPIKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA POLISI VWAWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA. WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO. MNAMO TAREHE 11.08.2013 MAJIRA YA SAA 16:10HRS HUKO ENEO LA CCM BARABARA YA MBEYA/IRINGA JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI T.815 ABQ AINA YA TOYOTA HILUX LIKIENDESHWA NA DEREVA LUSAJO S/O ASAJILE, MIAKA 37, KYUSA, MKAZI WA ITUHA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MAKA S/O MWAMWINGA, MIAKA 12, KYUSA, MKAZI WA ILOMBA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. WILAYA YA MBARALI – KUPATIKANA NA SILAHA BILA KIBALI. MNAMO TAREHE 11.08.2013 MAJIRA YA SAA 16:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAHONGOLE WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA STEVEN S/O MTOVANGWA,MIAKA 65,MHEHE,MKULIMA ,MKAZI WA KIJIJI CHA MAHONGOLE AKIWA ANAMILIKI SILAHA MOJA AINA YA SHORT-GUN ISIYOKUWA NA NAMBA AKIIMILIKI KINYUME CHA SHERIA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUHAKIKISHA KUWA WANAMILIKI SILAHA KWA KUFUATA TARATIBU ZILIZOWEKWA KISHERIA VINGINEVYO SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE. [ DIWANI ATHUMANI - ACP ] KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE   12. 08. 2013.


WILAYA YA  MBOZI – AJALI YA  PIKIPIKI KUGONGANA  NA
                                                               KUSABABISHA KIFO
.


MNAMO TAREHE 11.08.2012 MAJIRA YA  SAA 17:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA WASA KATA YA  MSIA WILAYA YA  MBOZI  MKOA WA MBEYA.  PIKIPIKI  T.225 BNY NA T.758 CCC ZOTE AINA YA  T-BETTER  ZILIGONGANA NA KUSABABISHA MWENDESHA PIKIPIKI MMOJAWAPO AITWAE ADAM S/O SIMKOKO, MIAKA 27, MNYIHA, MKAZI WA KIJIJI CHA WASA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA  WILAYA YA  MBOZI. CHANZO NI MWENDO KASI KWA WAENDESHA PIKIPIKI WOTE WAWILI. MWENDESHA PIKIPIKI WA PILI HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE BAADA YA  KUKIMBIA MARA BAADA YA  TUKIO NA KUITELEKEZA PIKIPIKI YAKE ENEO LA TUKIO. PIKIPIKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA POLISI VWAWA.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.


WILAYA YA  MBEYA MJINI – AJALI YA  GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
                                                        KUSABABISHA KIFO.



MNAMO TAREHE 11.08.2013 MAJIRA YA  SAA 16:10HRS HUKO ENEO LA CCM BARABARA YA  MBEYA/IRINGA JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI T.815 ABQ AINA YA  TOYOTA HILUX LIKIENDESHWA NA DEREVA LUSAJO S/O ASAJILE, MIAKA 37, KYUSA, MKAZI WA ITUHA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MAKA S/O MWAMWINGA, MIAKA 12, KYUSA, MKAZI WA ILOMBA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI.  MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


WILAYA YA  MBARALI – KUPATIKANA NA SILAHA BILA KIBALI.


MNAMO TAREHE 11.08.2013 MAJIRA YA  SAA 16:00HRS  HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAHONGOLE WILAYA YA  MBARALI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA STEVEN S/O MTOVANGWA,MIAKA 65,MHEHE,MKULIMA ,MKAZI WA KIJIJI CHA MAHONGOLE AKIWA ANAMILIKI SILAHA MOJA AINA YA  SHORT-GUN  ISIYOKUWA NA NAMBA AKIIMILIKI KINYUME CHA SHERIA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUHAKIKISHA KUWA WANAMILIKI SILAHA KWA KUFUATA TARATIBU ZILIZOWEKWA KISHERIA VINGINEVYO SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE.



 [ DIWANI ATHUMANI  - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


WILAYA YA KYELA – WATUHUMIWA SITA WALIODHIBITIWA NA WAUMINI KWA USHIRIKIANO NA MAKACHERO WA POLISI KWA KUFANYA FUJO MSIKITINI WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KESHO TAREHE 12.08.2013.


NYONGEZA YA TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE   11. 08. 2013.



MNAMO TAREHE 12.08.2013  ASUBUHI WATUHUMIWA SITA WAUMINI WA DINI YA  KIISLAMU WALIOFANYA  FUJO KATIKA MSIKITI MKUU WA IJUMAA WILAYA YA  KYELA NA KUDHIBITIWA WANATARAJIA KUFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA YA  WILAYA YA  KYELA NA KUSOMEWA MASHTAKA BAADA YA  TARATIBU ZA UPELELEZI KUKAMILIKA, MIONGONI MWA MASHITAKA HAYO NI PAMOJA NA  SHAMBULIO NA KUJERUHI.

AWALI MNAMO TAREHE 09.08.2013 MAJIRA YA SAA 08:30HRS HUKO ENEO LA BONDENI KATIKA MSIKITI MKUU WA IJUMAA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. NURU S/O MWAFILANGO,MIAKA 77,KYUSA,SHEKHE MKUU WA WILAYA YA  KYELA, MKAZI WA BONDENI  AKIWA ANAONGOZA IBADA YA  SWALA YA    IDD EL FITRI  MSIKITINI HAPO ALIVAMIWA NA BAADHI YA  WAUMINI WANAOJIITA WAISLAM WENYE ITIKADI KALI NA KUANZA KUMSHAMBULIA KWA KUTUMIA FIMBO,NONDO,MKASI NGUMI NA MATEKE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE. CHANZO NI KUWA HAWAMTAKI SHEKHE HUYO KWA MADAI KUWA HANA UWEZO. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMVAMIA MHANGA WAKATI WAUMINI WOTE WAKIWA  WAMEINAMA WAKISWALI NA KUANZA KUMSHAMBULIA. MHANGA HAKUPATA MADHARA BAADA YA BAADHI YA WAUMINI WALIOSHIRIKIANA NA POLISI/MAKACHERO WA KIISLAMU KUMUOKOA. KUFUATIA TUKIO HILO WATUHUMIWA SITA AMBAO WALIKUWA VINARA WA VURUGU HIZO WALIKAMATWA AMBAO NI 1. MASHAKA S/O KHASIMU, MIAKA 30, MUHA, MKULIMA MKAZI WA NDANDALO 2. ISSA S/O JUMA, MIAKA 37, MRANGI, MKULIMA, MKAZI WA BONDENI 3. AHMED S/O KHASIMU @ MAGOGO, MIAKA 35, MPOGORO, MKULIMA/MGANGA WA KIENYEJI, MKAZI WA MBUGANI [ALIKUTWA NA MKASI] 4. IBRAHIM S/O SHABAN, MIAKA 17, KYUSA, MWANAFUNZI SHULE YA  SEKONDARI KYELA DAY KIDATO CHA NNE MKAZI WA NDANDALO [ALIKUTWA NA FIMBO KUBWA NA NDIYE ALIYEMNYANG’ANYA SHEKHE KIPAZA SAUTI] 5. AMBOKILE S/O MWANGOSI @ ALLY, MIAKA 19, KYUSA, MWANAFUNZI WA SHULE YA  SEKONDARI  KYELA DAY KIDATO CHA TATU, MKAZI WA BONDENI [ALIKUTWA NA KIPANDE CHA NONDO] NA 6. SADICK S/O ABDUL, MIAKA 28, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA NDANDALO. AIDHA  KATIKA TUKIO HILO HAMIS S/O HUSSEIN, MIAKA 50, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA BONDENI ALIPATA MAJERAHA KIDOGO KWA KUKATWA MKASI  JUU YA  SIKIO LA KUSHOTO WAKATI AKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUMUOKOA MHANGA  ASIPATE MADHARA  NA AMEPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA. HALI YA USALAMA NA AMANI ILIREJEA MUDA MFUPI NA WAUMINI WALIENDELEA NA IBADA YAO CHINI YA UONGOZI WA SHEKHE HUYO NA KUMALIZA SALAMA. HAKUNA UHARIBIFU WA MALI ULIOTOKEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA WAUMINI NA JAMII KWA UJUMLA KUTATUA MATATIZO/KERO/MALALAMIKO YAO KWA NJIA YA   KUKAA  KWENYE  MEZA YA  MAZUNGUMZO BAADA YA   KUYAWASILISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA  ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANASISITIZA KUWA YEYOTE ATAKAYEJARIBU/ATAKAYEVUNJA SHERIA AWE NI KIONGOZI/MUUMINI WA DINI YEYOTE, AWE NI KIONGOZI WA SIASA, AWE NI MFANYABIASHARA N.K. HATAFUMBIWA MACHO.



 [ DIWANI   ATHUMANI  - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.